Saturday 18 March 2017

Muungano wa Madaktari wa Kenya, Wakosoa Madaktari wa Tanzania Kufanya Kazi Kenya

by on 23:26

Muungano wa Madaktari Kenya (The Kenya Medical Practitioners and Dentists Union - KMPDU) umepinga hatua ya serikali kuajiri madaktari toka Tanzania.

Wanasema kama Serikali ya Kenya wanahitaji Madaktari, wawaajiri kwanza madaktari 1,400 waliomo Nchini Kenya.

Tanzania imetoa Madaktari 500 kuitikia ombi la rais wa Kenya Uhuru Kenyata.

Hivi karibuni Kenya ilikumbwa na Mgomo mkubwa wa Madaktari wakishinikiza nyongeza ya Mshahara.


Source:

KMPDU Secretary General Ouma Oluga Criticises Government for Bringing Doctors From Tanzania

By JULIET MUTAHI

Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists Union (KMPDU) Secretary General Ouma Oluga, has issued a new demand after Tanzanian President John Magufuli offered to send 500 doctors to Kenya.

Oluga demanded that the foreign medics must go through several procedures including undergoing an examination before they start working in the country.

The Secretary General criticised the government for seeking outside help yet there were many unemployed medical practitioners in Kenya.

He wondered why the government had to source for doctors from Tanzania yet it would pay the same money the local medics had been demanding for.

"Kenya has about 1,400 doctors awaiting employment. It would be very costly and therefore a show of imprudent public finance management to have 500 Tanzania doctors at Sh20,000 per day," he said.

At the same time, Dr Oluga accused the government of failure to retain doctor's in hospitals due to lack of proper working conditions.

He, however, assured that KMPDU would welcome the foreign practitioners and register them into the Union.

Earlier in the day, Magufuli had agreed to offer the 500 medics to help mitigate the effects of the recently called off strike following a request by President Uhuru Kenyatta.

He stated that there were many qualified and unemployed doctors who were ready to offer their services in Kenya.

Source: Government Issued New Demand After Magufuli Gives Kenya 500 Doctors

Friday 17 March 2017

Maneno 19 ya Jerry Muro kwa kocha Hans van Pluijm baada ya kusaini Singida United

by on 06:48
 Baada ya kutangaza kuvunjwa mkataba Dar es Salaam Young Africans na kocha wake wa zamani ambaye walimpatia majukumu mapya ya kuwa mkurugenzi wa ufundi raia wa Uholanzi Hans van Pluijm, leo March 17 2017 timu ya Singida United iliyopanda kucheza Ligi Kuu imempa mkataba wa miaka miwili kocha huyo.
                                                               Jerry Muro

 Baada ya taarifa hizo kuenea aliyekuwa afisa habari wa Yanga Jerry Muro ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe unaotafsirika kama kumfariji kocha Hans van Pluijm “Babu Hans pumzika hapo kwa muda, wapiga dili wanaomdanganya muhindi wakishaondoka kule, tutarejea tu hata kwa mlango wa uani”

 Kuondolewa kwa Hans van der Pluijm akiwa kaipatia Ubingwa wa Ligi Kuu na FA Yanga msimu uliyopita sambamba na kuiwezesha kufika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, kumewashangaza wengi kutokana na kutoona sababu za msingi za kumuondoa Hans

Tundu Lissu afikishwa mahakamani ......Asomewa mashitaka Matano na Kuachiwa Kwa Dhamana

by on 06:30

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana Mbunge Tundu Lissu aliyefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matano.

Lissu amesomewa Mashitaka matano(5)  ambayo ni yale yale aliyofutiwa hapo awali kuhusu maneno ya Uchochezi kwenye Uchaguzi wa Dimani,Zanzibar.

Serikali imesema upelelezi umekamilika na   ikaomba kesi ianze kusikilizwa leo.Lissu aliiomba mahakama isisikilize  kesi hii  leo ili akashiriki Uchaguzi wa TLS utakaofanyika kesho mkoani Arusha.

Mahakama imekubali maombi ya Tundu Lissu na kumwachia huru kwa dhamana ya milioni 10 ambapo tayari amekwishapanda ndege kuelekea jijini Arusha Kushiriki Uchaguzi huo

Breaking News: Rais Magufuli Afuta Agizo La Kufunga Ndoa Kwa Sharti La Kuwa Na Cheti Cha Kuzaliwa

by on 01:59

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa jana tarehe 16 Machi, 2017 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa watu wote watakaofunga ndoa kuanzia tarehe 01 Mei, 2017.

Rais Magufuli amefuta agizo hilo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi kabla ya kuondoka katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema Serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.

Amesema mpaka sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.

“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe” Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi.

Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupata vyeti vyao vya kuzaliwa kama kawaida na amewataka viongozi wote kuwahamasisha wananchi kuwa na vyeti hivyo.


Thursday 16 March 2017

Serikali yapiga marufuku kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa

by on 12:04

Serikali  imepiga marufuku watu kufunga ndoa bila kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hayo leo akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.

Pamoja na mambo mengine, Dk.Mwakyembe amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na Vifo (RITA), kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema kuwa bila kuwa na  takwimu sahihi  za  vizazi na vifo ama ndoa  inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.

“Wenzetu nchi zilizoendelea suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi bado tuko nyuma, kwa mfano Mkoa wa Morogoro  kwa mujibu wa sensa  ya watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti  vya kuzaliwa ni asilimia 11 pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,” amesema.

Dk. Mwakyembe pia ametumia nafasi hiyo kuwaonya watendaji wa mahakama watakaolalamikiwa na wananchi kufanya kazi kinyume na maadili ikiwamo upokeaji wa rushwa ama kutotenda haki na kutumia  mahakama kugeuza kesi za madai kuwa kesi za jinai.

Diamond Platnumz na Alikiba Ndani ya Wimbo Mmoja....

by on 11:57

KUELEKEA fainali ya kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Gabon, kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys inayoongozwa na Mwenyekiti Charles Hilal imeandaa wimbo wa pamoja utakaoimbwa na wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseebb Abdul ‘Diamond’ na Ali  Saleh ‘King Kiba' pamoja na wasanii wengine.

Wimbo huo wa pamoja ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha kampeni za kuchangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys itakayofanyika mwezi wa tano nchini Gabon ambapo zitapatikana nchi nne zitakazokwenda kombe dunia la vijana nchini India.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Charles Hilal amesema kuwa kwa pamoja wimbo utakaowahusisha wasanii wengine mbalimbali utakuwa na lengo kuu la kuhamasisha wananchi, wadau na wapenda michezo kuichangia timu hiyo ya vijana kwa lengo la kuisaidia malengo waliyokuwa wameyafikia ya kuipeleka timu hiyo kwenye fainali za kombe la Dunia nchini India.

Hilal amesema kuwa hatua hii ya kusaidia Serengeti Boys kutawajenga vijana hawa kufanya vizuri katika michuano ya mataifa Afrika kwa vijana ikiw ani pamoja na kupata kambi nje ya nchi na kuchgeza mechi kadhaa za kirafiki kutoka nchini jirani lakini hata hivyo bado wanafikria kutafuta mechi ya kirafiki itakayochezwa hapa hapa Jijini Dar es salaam ikiwa ni kwa ajili ya kuwaaga kuelekea nchini Gabon.

Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge amesema kwamba tayari ala za wimbo huo zimekwishatengenezwa na wasanii hao wote wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti, ili mara moja wimbo huo ukamilishwe na kuanza rasmi kusaidia kampeni ya kuhamasisha Serengeti Boys.

“Tayari wasanii Ali kiba na Diamond wameshakubali kurekodi nyimo hiyona wameahidi kufanya haraka kuingiza sauti kwenye ala ambazo tumeshawatumia na baadae wasanii wengine kama Mwasiti Almasi, Darasa na Vanesa Mdee nao wataweka sauti zao,"amesema Kitenge.

Kiba na Diamond wote wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia Serengeti Boys iliyofuzu Fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.

Katibu wa Kamati hiyo ni Mwesigwa Selestine ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Kitenge wa EFM Radio na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu, yumo Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.

Pia, Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa kila hatua kuanzia Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya Hamasa kwa lengo la kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.

 Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya Serengeti Boys kueleka kwnye kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17 yatakayofanyika nchini Gabon. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano

Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akiwa pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge wakiwasikilizisha waandishi ala za wimbo unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya kuhamasisha kuichangia Serengeti Boys

Meya wa Ubungo Kufungua Kesi Dhidi ya Vyeti Feki..!!!

by on 07:43

 Mayor wa Ubungo Mh. Borniface Jacob anakusudia kufungua shauri mahakamani la kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuonesha vyeti vyake ili kuondoa utata uliojitokeza hivi karibuni dhidi ya kiongozi huyo wa mkoa. Kesi hiyo inatarajiwa kufunguliwa jumatato ijayo ya tar 20/03/2017.