Wednesday 15 March 2017

Baada ya kuwa nje ya uwanja ndani ya miezi sita Essien amepata Timu

 Staa wa zamani wa Chelsea ya England na Real Madrid ya Hispania Michael Essien March 14 2017 ametangaza kujiunga rasmi na timu ya Persib Bandung ya Indonesia baada ya kuwa nje ya uwanja bila timu kwa miezi sita.
Essien alikuwa hana timu kwa kipindi cha miezi sita baada ya kuachana  na Panathinaikos ya Ugiriki mwaka 2016 na amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha akiba cha Chelsea kabla ya kujiunga na Persib Bandung.
Michael Essien mwenye umri wa miaka 34 alikataa kujiunga  na Melbourne ya Australia mwezi December mwaka jana, Essien amewahi kuichezea Chelsea ya England kwa misimu nane.
image

No comments:

Post a Comment